IQNA

Iran yatoa  pendekezo la Kuanzishwa  Sekretarieti ya Kimataifa kwa Mashindano ya Qur’an Tukufu 

10:50 - February 09, 2025
Habari ID: 3480184
IQNA - Iran inafikiria kutoa pendekezo la kuanzisha sekretarieti ya kimataifa kwa waandaaji wa mashindano ya Qur’ani Tukufu  ya kimataifa ili kukuza ushirikiano kati ya nchi zinazohost mashindano hayo.

Mohammad Ridha  Pourmoein, mshauri wa Sekretarieti ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran, alizungumza na IQNA kuhusu pendekezo hilo.

Kwa mujibu wa Pourmoein, pendekezo hilo kwa sasa linakaguliwa na mamlaka husika ndani ya Iran, ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na mkuu wa Shirika la Awqaf na Mambo ya Hisani.

 Ikiwa litaidhinishwa, Sekretarieti hiyo itafanya kazi kupitia kamati maalum zinazozingatia maeneo kama vile uchapishaji, mafunzo ya kiufundi na kitaaluma, kubadilishana wasomi wa Qur’an, uamuzi wa mashindano, kutambua wachangiaji mashuhuri, pamoja na usimamizi na tathmini, kwa mujibu wa mshauri huyo.

Jua Sheria, Boresha Alama Yako: Jaji Atoa Vidokezo kwa Wanaoshindana katika Mashindano ya Qur’an

 Pourmoein alielezea faida kadhaa zinazotarajiwa kutokana na kuanzishwa kwa sekretarieti hii. Hizi ni pamoja na uratibu bora katika kuandaa matukio ya Qur’ani, maendeleo ya mbinu zilizosanifishwa, kubadilishana mbinu bora na utaalamu, kutuma wataalam wa Qur’ani katika nchi mbalimbali, na uwezekano wa kuanzishwa kwa vyuo vya kitaaluma na kiufundi vilivyojitolea kwa masomo ya Qur’ani.

 Pendekezo hili linakuja kufuatia toleo la 41 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran, ambayo yalifanyika mwezi uliopita katika mji wa Mashhad, mji maarufu wa kidini na kitamaduni kaskazini-mashariki mwa Iran.

Mashindano hayo, yanayotambulika kama mojawapo ya matukio ya Qur’ani yenye heshima zaidi duniani, yalikusanya washiriki 57 kutoka nchi 27, wakionyesha ubora katika usomaji na kuhifadhi Qur’ani.

Mtaalam wa Iraq aonyesha Kinachotofautisha Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran na Yale ya Nchi Nyingine

 Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani  ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanaandaliwa kila mwaka na Shirika la Awqaf na Mambo ya Hisani la nchi hiyo.

 Mashindano haya yanakusudia kukuza utamaduni na maadili ya Qur’an miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani Tukufu.

 

3491796

 

 

 

Kishikizo: Qur'an tukufu wasomi
captcha